China na Afrika kutotenganishwa kutokana na mshikamano na ushirikiano wao mzuri
2021-12-03 09:41:46| cri

China na Afrika kutotenganishwa kutokana na mshikamano na ushirikiano wao mzuri_fororder_timg (2)

Hivi karibuni waziri wa mambo ya nje wa Marekani Anthony Blinken alitembelea nchi tatu za Afrika, Kenya, Nigeria na Senegal. Katika ziara hiyo, alijaribu tena kuichafua matope China ili kuimarisha ushawishi wa Marekani barani Afrika, lakini China na Afrika haziwezi kutenganishwa kutokana na mshikamano na ushirikiano wao mzuri.

Katika ziara hiyo, Blinken alisema “Marekani imerudi”, akidai kwamba mikataba ya ujenzi wa miundombinu kati ya Afrika na “baadhi ya nchi” huzifanya nchi za Afrika kushindwa kudhibiti madeni, ila wachambuzi wengi wanaamini kuwa, kauli hiyo inalenga pendekezo la China la “Ukanda Mmoja, Njia Moja”.

Lakini kama Blinken alivyohisi barani Afrika, mshikamano, urafiki na ushirikiano wa karibu kati ya China na Afrika ni vitu visivyoweza kupuuzwa. Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Geoffrey Onyeama alimjibu Brinken moja kwa moja, akisema fursa kubwa katika ushirikiano na China zinaonekana, nchi ambayo ina uzoefu mkubwa katika miradi mikubwa ya uhandisi na miradi ya miundombinu. Gazeti la Citizen la Afrika Kusini limesema, Marekani ni nchi yenye uchumi mkubwa zaidi duniani, lakini hali hii haimaanisha nchi hiyo inaweza kuwafundisha viongozi wa nchi za Afrika namna ya kufanya, na nchi za Afrika zina haki ya kuchagua marafiki zake.

Kwa miaka mingi iliyopita, China imekuwa na ushirikiano mzuri na nchi za Afrika katika nyanja mbalimbali, na kupata mafanikio mengi makubwa. Kwa upande wa biashara, China imeendelea kuwa mwenzi mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 12 mfululizo. Tangu kuanzishwa kwa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), thamani ya biashara kati ya pande hizo mbili imeongezeka na kufikia dola bilioni 200 za Kimarekani mwaka 2020 kutoka dola bilioni 10 ya mwaka 2000, na kuongezeka kwa mara 20. Kwa upande wa miundombinu, Afrika imekuwa soko la pili la China kwa miradi ya ujenzi wa miundombinu katika nchi za nje. China imetekeleza miradi mingi ya miundombinu kwa kuendana na mahitaji ya nchi za Afrika. Takwimu zinaonyesha kuwa, tangu kuanzishwa kwa FOCAC, makampuni ya China yameongeza na kuboresha zaidi ya kilomita 10,000 za reli na karibu kilomita 100,000 za barabara barani Afrika, na kutoa nafasi zaidi ya milioni 4.5 za ajira kwa wenyeji katika nchi husika. Uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika umezidi dola bilioni 43.4, za kimarekani, na kushika nafasi ya nne kwa ukubwa wa uwekezaji barani Afrika.

Sasa tujiulize, nani ni rafiki wa kweli wa Afrika? Hapa kuna jibu. Ripoti iliyotolewa hivi karibuni na shirika maarufu la uchunguzi wa maoni la Afrika la Afrobarometer inaonesha kuwa, ushawishi wa China barani Afrika unashika nafasi ya kwanza duniani, mbele ya Marekani, mashirika ya kikanda, mashirika ya Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika. Haya ni matokeo ya ushirikiano wa dhati kati ya China na Afrika kwa miaka mingi.

Kitu kinachohitajika na Afrika ni uaminifu, sio mahesabu. Marekani inapaswa kusikiliza ushauri wa mtaalamu wa Afrika Kusini Eric Orland, ambaye amesema kushindana na China kila wakati ni mchezo unaoelekea kushindwa kwa serikali ya Marekani, ambayo inapaswa kuzingatia hatua zake zinazoweza kuisaidia Afrika kihalisi.