Afrika yapaswa kusawazisha malengo na vitendo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali
2021-12-03 08:58:31| cri

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amesema, bara la Afrika linakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile janga la COVID-19, amani na usalama, na linapaswa kusawazisha malengo na hatua zake ili kukabiliana na changamoto hizo.

Bw. Guterres alisema kuondokana na janga la COVID-19 ni moja ya mambo muhimu katika kufufua uchumi barani Afrika. Ingawa Umoja wa Afrika umejitahidi kuongeza upatikanaji wa chanjo na vifaa tiba,  ni asilimia 6 tu ya watu wa Afrika ndio wamepatiwa chanjo kamili.

Bw. Guterres pia amesema hivi sasa Ethiopia, Sudan, eneo la Sahel na Jamhuri ya Afrika ya Kati, bado zinakumbwa na changamoto kubwa za amani.