China yatoa waraka wa Demokrasia nchini China
2021-12-04 12:55:30| cri

Ofisi ya habari ya Baraza la Serikali la China leo limetoa waraka wa Demokrasia nchini China, ambao umeeleza mawazo ya China kuhusu thamani ya demokrasia, mfumo na utekelezaji wa mambo ya demokrasia nchini China, mafanikio yaliyopatikana na mchango uliotolewa na China katika kuhimiza demokrasia.

Waraka huo unasema demokrasia ni thamani ya pamoja ya binadamu wote, na pia ni mawazo yanayoshikiliwa na Chama cha Kikomunisti cha China na watu wa nchi hiyo.

Waraka huo umesisitiza kuwa demokrasia ni haki ya watu wa nchi zote duniani, si haki maalumu kwa watu wa nchi chache tu, na badala ya nchi chache za nje kunyosha vidole, hali ya utekelezaji wa demokrasia katika nchi moja inapaswa kuthaminiwa na wananchi wake na jamii ya kimataifa kwa pamoja.