Iran yasema Marekani inapaswa kuchukua hatua mwanzo katika kufufua makubaliano ya nyuklia
2021-12-06 08:28:45| cri

Shirika la habari la Iran IRNA limeripoti kuwa Mpatanishaji mkuu wa masuala ya nyuklia ya Iran Ali Bagheri Kani amesema Marekani inapaswa kuchukua hatua mwanzo katika kufufua makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kwa kuwa yenyewe ndio imejiondoa kwenye makubaliano hayo.

Kwa mujibu wa ripoti Bw. Kani amebainisha kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran haitarudi nyuma juu ya matakwa yake ya kuondoa vikwazo katika mchakato wa kurejesha makubaliano ya nyuklia (JCPOA). Amesisitiza kuwa maombi yaliyotolewa na Iran kwa nchi nne jumlisha moja yaani Uingereza, China, Ufaransa, Russia jumlisha na Ujerumani kwenye mazungumzo ya hivi karibuni yaliyofanyika Vienna yamewekwa kumbukumbu na ni ya mantiki hivyo yanaweza kuwa msingi wa mazungumzo.

Baada ya mazungumzo hayo kukwama kwa miezi sita, Iran na nchi zilizosalia kwenye makubaliano, huku Marekani ikishiriki kwa njia isiyo ya moja kwa moja, zilianza mazungumzo yao ya kurejesha makubaliano Novemba 29.