Idadi ya watu waliokufa kwenye ajali ya basi lililoanguka mtoni yaongezeka hadi 32 nchini Kenya
2021-12-07 09:30:36| cri

Idadi ya vifo vya watu waliopata ajali ya basi lililokuwa limebeba abiria takriban 50 na kuanguka Jumamosi kwenye Mto Enziu ulioko kaunti ya Kitui, mashariki mwa Kenya imeongezeka hadi 32 .

Naibu kamanda wa eneo la Mwingi Bw. Joseph Yakan amesema waokoaji wamewaokoa watu 17 waliomo ndani ya basi. Miili kadhaa imepatikana mtoni Jumapili, na kufanya idadi ya vifo vya watu ifikie 32. Amesema basi hilo lilikuwa likijaribu kuvuka daraja lililokumbwa na mafuriko na kusombwa na maji njiani baada ya kuzidiwa na mawimbi.