China kudumisha ufunguaji mlango wenye kiwango cha juu
2021-12-07 09:48:34| cri

Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amesema uchumi wa China umeunganishwa kwa kina na uchumi wa dunia, na ufunguaji mlango ni chaguo la kutimiza maendeleo lililofanyika kwa kujiamulia, na China itafungua mlango wazi zaidi.

Li amesema hayo aliposhiriki Mkutano wa sita wa mazungumzo ya wakuu wa mashirika muhimu ya uchumi ya kimataifa uliofanyika jana kwa njia ya video.

Kwenye mkutano huo Li ameeleza kuwa huu ni mwaka wa 20 tangu China ijiunge na Shirika la Biashara Duniani WTO. Katika miaka 20 iliyopita, China imekuwa ikifuata kwa makini kanuni, kutekeleza kwa makini ahadi, ambapo imejiendeleza huku ikinufaisha dunia. Pia itafuata kanuni za kimataifa za uchumi na biashara zenye kiwango cha juu, kutoa ombi la kujiunga na Makubaliano ya Uhusiano wa Wenzi wa Kuvuka Pasifiki CPTPP, na Mkataba wa Ushirikiano wa Uchumi wa Kidijitali DEPA, pia itadumisha ufunguaji mlango katika kiwango cha juu, ili kuiwezesha dunia inufaike na fursa mpya za maendeleo ya China.