Uongozi wa CPC waitisha mkutano kuhusu kazi ya uchumi ya mwaka 2022, kupambana na ufisadi na nidhamu ya chama
2021-12-07 09:40:28| cri

Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC jana Jumatatu iliitisha mkutano wa kuchambua na kuchunguza kazi ya uchumi ya mwaka 2022, kupanga mwenendo wa chama na kazi ya kupambana na ufisadi, na kupitia kanuni zinazohusiana na ukaguzi wa nidhamu ya chama cha CPC.

Mkutano huo ambao umeongozwa na katibu mkuu wa Kamati Kuu ya CPC Xi Jinping, umesema mwaka 2021 umepiga hatua muhimu kwa Chama na taifa, na kuelezea mwitikio tulivu na wa ufanisi wa China kwenye mabadiliko na majanga ya dunia ambao haujaonekana kwa karne nzima, kukamilika kwa kazi kubwa ya mageuzi na maendeleo na kuanza vizuri kwa Mpango wa 14 wa Miaka Mitano.

Mkutano huo umetaka kazi ya uchumi kufanyika kwa njia imara chini ya mwongozo wa Mawazo ya Xi Jinping juu ya Ujamaa wenye umaalumu wa China katika zama mpya, na mwitikio wa COVID-19 kuratibiwa na maendeleo ya uchumi huku yakiboresha maisha ya watu.