Nchi za Afrika zatakiwa kuiga maendeleo ya Rwanda kwa kuweka mfumo maalumu wa utawala wa nchi
2021-12-07 09:47:29| cri

Mafanikio ya maendeleo ya Rwanda yaliyopatikana hivi karibuni yanaonesha haja ya nchi za Afrika kuweka vielelezo maalumu vya muundo wa serikali.

Costantinos Bt. Costantinos, profesa wa sera za umma katika Chuo Kikuu cha Addis Ababa Ethiopia, ameliambia Shirika la Habari la China Xinhua kwenye mahojiano ya hivi karibuni kuwa nchi za Afrika zinapaswa kuchambua hali yao ya jumla kabla ya kuanza kuweka kielelezo cha utawala ambacho kinafaa vizuri njia yao ya kina.

Msomi huyo ambaye alikuwa mshauri wa mambo ya uchumi katika Kamati ya Umoja wa Afrika na Kamati ya Uchumi ya Umoja wa Mataifa katika Afrika, ameitaja Rwanda kama mfano mzuri katika kuweka mfumo maalumu wa nchi ambao unapelekea maendeleo ya uchumi na jamii ya nchi hiyo.