Biden na Putin waongea kuhusu ushirikiano wa pande mbili, mgogoro wa Ukraine na makubaliano ya nyuklia ya Iran
2021-12-08 08:54:01| cri

Rais wa Marekani Joe Biden na mwenzake wa Russia Vladimir Putin jana Jumanne waliongea kwa njia ya video wakigusia masuala mbalimbali ya pande mbili pamoja na mgogoro wa Ukraine na makubaliano ya nyuklia ya Iran.

Rais Biden alielezea wasiwasi mkubwa wa Marekani na washirika wake wa Ulaya kuhusu Russia kuongeza vikosi vyake kuizunguka Ukrain na kumueleza wazi kwamba Marekani na washirika wake watajibu kwa kuchukua hatua kali za kiuchumi na nyinginezo dhidi ya tukio hilo. Biden pia amesisitiza kuunga mkono uhuru na mamlaka ya eneo la Ukraine na kutoa wito wa kupunguza nguvu za kijeshi na kurejea kwenye njia za kidiplomasia.

Naye rais Putin amemjibu Biden akitumia mfano wa “sera ya maangamizi” ya mamlaka ya Ukraine na kueleza wasiwasi mkubwa kuhusu vitendo vya uchokozi vya Kiev dhidi ya Donbass. Hivyo amesisitiza kuwa ni NATO ndio inayotaka kunyakua eneo la Ukraine na inajenga jeshi lake karibu na mipaka ya Russia.