Balozi Gert Grobler: China inayopenda kusikiliza sauti za Afrika ni mwenzi aliye sawa kwa Afrika
2021-12-08 15:46:58| CRI

Mwanadiplomasia mwandamizi wa Afrika Kusini Balozi Gert Grobler amesema, sifa maalumu ya Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) ni mwendelezo wa mawasiliano na mashauriano kati ya serikali na kwenye ngazi zisizo za kiserikali, ambayo yanayoshirikisha watendaji kwenye ngazi zote, na hatimaye kuweka ajenda na kufikia mwafaka kuhusiana na masuala yanayofuatiliwa kwa pamoja. Anaona, hatua za ushirikiano kama hizo zinaeleweka na kukubalika kwa upande wa Afrika, na pia zimethibitisha kuwa China ni mwenzi aliye sawa kwa Afrika, kwa kuwa “inasikiliza sauti za Afrika”.

Balozi Gert Grobler: China inayopenda kusikiliza sauti za Afrika ni mwenzi aliye sawa kwa Afrika_fororder_浙师大非洲研究院高级研究员、前南非驻外大使格特

Balozi Gert, ambaye pia ni mtafiti mwandamizi wa Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, hivi karibuni alipohojiwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China CMG, alimesema, kuanzia Mkutano wa kilele wa FOCAC uliofanyika mwaka 2018 mjini Beijing, hadi mkutano wa nane wa mawaziri uliofanyika mwezi Novemba mwaka huu huko Dakar, utekelezaji wa mipango ya utekelezaji ya FOCAC umedumisha mwendelezo pamoja na hatua zenye ufanisi za ufuatiliaji wa baadaye, na kuyageuza maamuzi yaliyofikiwa kwenye mikutano ya FOCAC kuwa matunda halisi yanayopimika. Anaona, utaratibu wa FOCAC umekuwa mfano wa kuigwa kwa ushirikiano wa kimataifa.

Amesema, mkutano wa Dakar ulipitia, kutathimini na kufuatilia hali ya utekelezaji wa maamuzi yaliyofikiwa kwenye mkutano wa kilele wa FOFAC uliofanyika mwaka 2018 mjini Beijing, ulijadili hatua za China na Afrika kupambana na janga la COVID-19, na kuweka mipango wakwa ajili ya maendeleo ya uhusiano kati ya China na Afrika katika miaka mitatu ijayo. Ameongeza kuwa, mkutano wa Dakar uliotoa matokeo halisi yanayotekelezeka na yanayotupia macho siku zijazo, umekubalika kwna viongozi wa Afrika kuwa “mafanikio kamili”.

Balozi Gert amesema, Miradi Tisa iliyotangazwa na Rais Xi Jinping kwenye mkutano wa Dakar imepongezwa sana na upande wa Afrika, kwa kuwa inahusisha na itatatua masuala, changamoto na ufuatiliaji wote wa Afrika uvinavyohusiana na maendeleo, ukuaji na ustawi wake katika siku za baadaye.

Anaona Ajenda ya Ushirikiano wa China na Afrika ya Mwaka 2035 iliyotangazwa na Rais Xi ni matunda yaliyopatikana kupitia mazungumzo, mashauriano na maandalizi ya pamoja kati ya China na Afrika. Mipango hiyo inaendana kwa karibu na mahitaji makuu ya Afrika ya kutimiza ukuaji wa uchumi, maendeleo endelevu na shirikishi, na ni ushahidi halisi wa kuthibitisha uhusiano wa enye usawa na kanuni ya kunufaishana kwenye ushirikiano kati ya pande hizo mbili.

Balozi Gert anaamini kuwa, kutokana na dhamira na uungaji mkono thabiti wa China, China na Afrika hakika zitaendelea kuimarisha hadhi, ushawishi na mshikamano wa FOCAC, na kupata mafanikio makubwa zaidi kwenye safari ya kuelekea kujenga Jumuiya yenye Hatma ya Pamoja kati ya China na Afrika.