Iran yatarajia nchi za Magharibi kuchukua hatua za kivitendo juu ya mazungumzo ya nyuklia
2021-12-08 08:54:26| cri

Mpatanishi mkuu wa Iran wa masuala ya nyuklia Ali Bagheri Kani amesema Iran imeingia kwenye duru mpya ya mazungumzo ya Vienna huku ikiwa na mapendekezo muhimu na ya kiujenzi na kutarajia hatua za kivitendo kuchukuliwa na nchi za Magharibi kuhusiana na suala hili.

Bw. Kani amesema katika duru mpya ya mazungumzo, yaliyoanza tena Novemba 29, Iran imetoa mapendekezo juu ya masuala ya kuondoa vikwazo na hatua za nyuklia, ambayo yanaweza kusukuma mbele mchakato wa mazungumzo hayo. Akielezea uhusiano baina ya Iran na Russia kama ni mzuri katika nyanja mbalimbali, Bagheri Kani amesema wameshauriana na Russia juu ya masuala mbalimbali na wameshashauriana na maafisa wa Russia kuhusu mazungumzo ya Vienna.

Mpatanishi huyo amesema anatumai kwenye mkutano ujao, mazungumzo yataendelea kwa haraka zaidi.