Watu wanne wafariki katika ajali ya jengo lililoporomoka jijini Dar es Salaam Tanzania
2021-12-08 08:55:58| cri

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Bw. Kheri James amesema kuwa watu wanne wamefariki na wengine 17 kujeruhiwa baada ya jengo la ghorofa moja kuporomoka Jumatatu jioni katika kata ya Goba manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam Tanzania.

Ameongeza kuwa wanawake wawili walifariki wakati jengo hilo lililokuwa likiendelea kujengwa kuporomoka kwenye nyumba mbili za jirani, na wanaume wawili ambao walikuwa sehemu ya timu ya wajenzi pia walifariki baada ya jengo hilo kuporomoka, pia amesema miongoni mwa watu 17 waliojeruhiwa kuna walio katika hali mbaya zaidi.

Aidha wachunguzi kutoka vyombo mbalimbali vya usalama wanajitahidi kubaini chanzo cha kuporomoka kwa jengo hilo, na baada ya uchunguzi huo eneo hilo litaondolewa vifusi.