Mjumbe wa IOC asema kususia kidiplomasia Michezo ya Olimpiki ya Beijing hakutaiathiri China
2021-12-09 15:01:54| cri

Mjumbe wa Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa IOC Dick Pound amesema kile kinachoitwa “kususia kidiplomasia” kwa Marekani dhidi ya Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Baridi ya Beijing ya mwaka 2022 hakutaleta athari kubwa.

Katika mahojiano aliyofanyiwa hivi karibuni na chombo cha habari cha Marekani Politico, makamu wa rais huyo wa zamani wa IOC Pound amesema ana mashaka kama hiyo inaweza kuchukuliwa ni kususia au la ikiwa maofisa wa Marekani hawakualikwa tangu mwanzo. Amesisitiza kuwa huwezi kususia shughuli ambayo hukualikwa.