Rais Xi Jinping asema China itaimarisha uhusiano na Ujerumani
2021-12-09 15:01:10| cri

Rais Xi Jinping wa China ametoa salamu za pongezi kwa Olaf Scholz kwa kuchaguliwa kwake kama kansela wa Ujerumani na kutoa wito wa kukuza uhusiano wa China na Ujerumani na kufikia kiwango kipya.

Ameongeza kuwa kwa kutumia fursa ya kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili mwaka ujao, China inapenda kuboresha na kuzidisha uaminifu wa kisiasa, kupanua mawasiliano na ushirikiano katika nyanja mbalimbali na Ujerumani. Rais Xi amesema kuwa China na Ujerumani ni washirika wa kimkakati wa pande zote, kwa miaka mingi, zimezingatia kuheshimiana, kutafuta maelewano ya pamoja na kuepusha tofauti na kutafuta ushirikiano wa pande zote, ambao umekuwa na matokeo ya kuzinufaisha nchi hizo mbili.