Marubani wanawake walivyoleta mapinduzi kwenye safari za anga zilizokuwa zikitawaliwa na wanaume pekee
2021-12-10 10:53:27| Cri

Tangu ndugu wawili Orville na Wilbur Wright warushe ndege ya kwanza mwaka 1903, anga imekuwa ikitawaliwa na wanaume pekee. Kwani watu wengi waliamini kwamba hii ni kazi ngumu inayohitaji maarifa na umakini wa wanaume. Lakini kadiri miaka inavyoyoyoma kumekuwa na mapinduzi makubwa kwenye safari za anga na sasa tunashuhudia sura mpya kabisa katika safari za angani. Leo hii kwenye kipindi cha Ukumbi wa Wanawake tutaangalia ujasiri na juhudi zilizochukuliwa na wanawake mbalimbali katika sekta hii ya urushaji ndege.