Baraza la Usalama lashindwa kuridhia azimio kuhusu hatari za kiusalama zinazohusiana na tabianchi
2021-12-14 09:29:12| CRI

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa jana lilikataa muswada wa azimio uliopendekeza kujumuisha hatari za kiusalama zinazohusiana na tabianchi, kama sehemu kuu ya mikakati ya kuzuia migogoro ya Umoja wa Mataifa inayolenga kusaidia kukabiliana na hatari ya kutokea tena kwa migogoro.

Katika upigaji kura kuhusu mswada huo, nchi 12 zilipiga kura ya ndiyo, na nchi mbili India na Russia zilipiga kura ya hapana, na China haikupiga kura. Baraza hilo limeikataa mswada huo kutokana na kura ya hapana ya mjumbe wa kudumu wa baraza la usalamaa.

Mswada huo ulitolewa na Niger ambayo ni nchi mwenyekiti wa zamu wa mwezi wa Disemba pamoja na Ireland. Upigaji kura ulifanyika baada ya mjadala wa wazi wa baraza hilo tarehe 9 mwezi Disemba ambapo wasemaji karibu 60 walionya kwamba watu na nchi zilizoathiriwa vibaya zaidi na mabadiliko ya tabianchi pia zitaathiriwa vibaya na ugaidi na ghasia.