Serikali ya Ethiopia yasema mkutano wa FOCAC ni wenye mafanikio
2021-12-15 09:48:22| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia Bw. Dina Mufti jana aliwaambia waandishi wa habari kuwa mkutano wa 8 wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) uliofanyika mwishoni mwa Novemba nchini Senegal una manufaa na mafanikio katika kuimarisha uhusiano kati ya China na Afrika.

Bw. Mufti amesema Ethiopia inaweza kunufaika kutokana na matokeo ya mkutano huo, China itaweka mfuko maalum wa kufungua njia yenye urahisi kwa ajili ya mauzo ya bidhaa za kilimo kutoka Afrika kwa nchi za nje na kutoa msaada wa fedha kwa usafirishaji wa bidhaa kutoka Afrika.