Rais Xi Jinping wa China asisitiza kujiamini kiutamaduni kwenye mkutano mkuu wa wasanii na waandishi
2021-12-15 09:03:12| CRI

Rais Xi Jinping wa China asisitiza kujiamini kiutamaduni kwenye mkutano mkuu wa wasanii na waandishi_fororder_1128163646_16394942815661n

Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito kwa wasanii na waandishi kuimarisha mwamko wao na kujiamini kwenye utamaduni wa China, kujenga mustakbali mpya kwa fasihi na sanaa ya China, na kuleta mwanga mpya kwenye utamaduni wa China.

Akiongea kwenye mkutano wa 11 wa taifa wa shirikisho la fasihi na sanaa, na mkutano wa 10 wa taifa wa jumuiya ya waadhishi wa China, Rais Xi amesema Chama cha Kikomunisti kimeongoza jumuiya ya fasihi na sanaa kwenye njia ya maendeleo kikiongozwa na U-marx unaoendana na mazingira ya China na utamaduni wa China, na kutoa kipaumbele kwa watu.

Rais Xi amesema watu wanaofanya kazi kwenye sekta ya fasihi na sanaa wanatakiwa kutumikia umma na ujamaa, na kufuata sera ya “maua 100 kuchanua, na mawazo 100 kutolewa” kuhimiza mageuzi yenye uvumbuzi na maendeleo, na kuweza kutekeleza majukumu na kazi.