Ripoti yaonesha ushirikiano wa uchapishaji kati ya China na nchi za “Ukanda Mmoja, Njia Moja” waimarishwa
2021-12-15 09:20:20| CRI

Ripoti kuhusu maendeleo ya ushirikiano wa uchapishaji wa “Ukanda Mmoja, Njia Moja” (juzuu ya tatu) iliyotolewa hivi karibuni na Taasisi ya Utafiti wa Habari na Uchapishaji ya China inaonesha kuwa katika kipindi cha 13 cha miaka mitano, idadi ya biashara ya hakimiliki kati ya China na nchi za Ukanda Mmoja, Njia Moja imeongezeka kutoka 3,808 ya mwaka 2016 hadi kufikia 10,729 ya mwaka 2020, na ushirikiano kwenye mambo ya uchapishaji kati ya pande hizo mbili umefikia kwenye kipindi cha kuinuka kwa ubora na ufanisi.