Sekta binafsi ya Tanzania kuimarisha ushiriki wa diaspora kwenye shughuli za uchumi
2021-12-16 09:11:37| CRI

Mfuko wa sekta binafsi wa Tanzania (TPSF) na kituo cha Diaspora cha Tanzania (TDH) wamesaini makubaliano kuhusu kuimarisha ushiriki wa watanzania wanaoishi nje kwenye shughuli za uchumi.

Taarifa iliyotolewa mjini Dar es salaam na TPSF inasema lengo la makubaliano hayo n kuwahimiza watanzania kuwekeza kwenye miradi, kuhimiza njia za kibiashara na kuhimiza maendeleo ya viwanda, pamoja na kuhimiza diplomasia ya uchumi.

Mkurugenzi wa TPSF Bw. Francis Nanai amesema watanzania 40 wanaoishi nje ya Tanzania wana nia ya kuwekeza Tanzania. Taarifa iliyotolewa inasema watanzania hao wana nia ya kuwekeza kwenye maeneo ya kuchakata mkonge, kilimo cha biashara, uchimbaji madini, usindikaji wa chakula, nishati na ufugaji wa samaki.

Mkurugenzi wa TDH Bw. Nassor Basalama amesema watanzania wanaoishi nje pia wanapenda kuwasaidia watanzania kupata elimu nje ya Tanzania na kutangaza vivutio vya utalii.