China na Russia zawa nguzo ya mfumo wa pande nyingi, na kushikilia haki na sheria
2021-12-16 09:12:10| CRI

China na Russia zawa nguzo ya mfumo wa pande nyingi, na kushikilia haki na sheria_fororder_HH3AIM6OMWM2$X3_(MLB4EU

Rais Xi Jinping wa China amesema China na Russia zimetekeleza kivitendo wajibu wa nchi kubwa, na kuwa kama nguzo ya kufuata mfumo wa pande nyingi na kushikilia kusimamia haki na sheria duniani.

Akiongea na mwenzake wa Russia Vladimir Putin kwa njia ya video ambao ni mkutano wa pili kati yao kwa njia ya video kwa mwaka huu na wa 37 tangu mwaka 2013, Rais Xi amesema katika nyakati tofauti Rais Putin ameupongeza ushirikiano kati ya China na Russia kama mfano wa kuigwa wa uratibu kati ya nchi katika karne ya 21, ameunga mkono maslahi makuu ya China, na kupinga kuchochea tofauti kati ya China na Russia.

Rais Xi pia amesema kumekuwa na mawasiliano na uratibu wa mara kwa mara kati yake ya Rais Putin kwa njia mbalimbali, na kuweza kuongoza kwa pamoja ushirikiano kati ya China na Russia.