“Miradi Tisa” yaongeza ubora na ufanisi wa ushirikiano kati ya China na Afrika
2021-12-16 14:35:00| CRI

Wanasiasa na wasomi wa nchi za Afrika watarajia mkutano wa Dakar wa FOCAC utainua ushirikiano wa Afrika na China kwenye kiwango kipya

Karibu tena msikilizaji kwenye kipindi hiki cha Daraja kinachokujia jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika kipindi cha leo msikilizaji, mbali na habari mbalimbali kuhusu China na Afrika, tutakuwa na ripoti itakayohusu Miradi Tisa iliyopendekezwa na China katika mkutano wa FOCAC uliofanyika mwishoni mwa mwezi uliopita na jinsi itakavyoongeza ubora na ufanisi wa ushirikiano kati ya China na Afrika. Pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi na Mkurungezi wa maswala ya Asia na Australia kwenye wizara ya mambo ya kigeni ya Kenya Bw. Paul Ndung’u.