NATO na EU zatoa mwito wa kupunguza mvutano kati ya Russia na Ukraine
2021-12-17 09:09:46| CRI

Jumuiya ya kujihami ya nchi za magharibi (NATO) imetoa mwito wa kupunguza majeshi ya Russia kwenye eneo la mpaka wa mashariki wa Ukraine, na kusema umoja huo utalinda ukamilifu wa ardhi ya Ukraine, huku ukitoa fursa ya majadiliano na Russia.

Katibu mkuu wa NATO Bw. Jens Stoltenberg amesema mjini Brussels baada ya kukutana na Rais wa Ukraine Bw. Volodymyr Zelenskyy kuwa wanatoa mwito kwa Russia kurudi kwenye diplomasia, kupunguza mvutano na kuheshimu uhuru na ukamilifu wa ardhi ya Ukraine, na kuonya kuwa uvamizi wowote dhidi ya Ukraine utakuwa na matokeo mabaya na kuwa na gharama kubwa.

Rais wa Ukraine amesema anapenda na anaamini kuwa njia ya kidiplomasia itakuwa na mafanikio.

Baadhi ya viongozi wa Umoja wa Ulaya pia wamerudia mwito walioutoa kwenye mkutano wao wa kilele wa mwaka jana. Waziri Mkuu wa Luxembourg amependelea Umoja wa Ulaya uialike Russia kwenye mkutano, na ofisa mkuu wa Umoja wa Ulaya anayeshughulikia sera za kidiplomasia na usalama Bw. Josep Borell amesema uvamizi wowote utakuwa na gharama kubwa ya kisiasa na kiuchumi.