Katibu Mkuu wa UM amesema mwakani amedhamiria kushughulikia zaidi janga na COVID-19 na changamoto za mfumo wa fedha
2021-12-17 09:10:32| CRI

Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Antonio Guterres amesema mwaka kesho amedhamiria kushughulikia upungufu kwenye usimamizi wa serikali katika mapambano dhidi ya janga la COVID-19 na mfumo wa fedha wa kimataifa.

Akiongea kwenye mkutano wake wa mwisho wa mwaka na wanahabari, Bw. Guterres amesema kuna changamoto kubwa kwenye kuzuia, kutambua na kukabiliana na majanga ya afya, na pia kuna changamoto kubwa kwenye mfumo wa fedha wa kimataifa.

Amesema amedhamiria kuwa mwaka 2022 utakuwa ni mwaka atakaoshughulikia changamoto za usimamizi wa serikali.

Lakini pia amesema nchi 40 duniani zimeshindwa kutoa chanjo kwa asilimia 10 ya watu wake, na kwenye nchi zenye mapato ya chini ni chini ya asilimia 4 tu ya watu ndio waliopata chanjo.