Kongamano la pili la Jumuiya ya Washauri Bingwa kati ya China na Sudan Kusini lafanyika kwa njia ya video
2021-12-19 09:35:43| CRI

Kongamano la pili la Jumuiya ya Washauri Bingwa kati ya China na Sudan Kusini lafanyika kwa njia ya video

Kongamano la pili la Jumuiya ya Washauri Bingwa kati ya China na Sudan Kusini lafanyika kwa njia ya video

Kongamano la pili la Jumuiya ya Washauri Bingwa kati ya China na Sudan Kusini lilifanyika Ijumaa Disemba 17 kwa njia ya video.

Chini ya uungaji mkono wa Ubalozi wa China nchini Sudan Kusini na Ubalozi wa Sudan Kusini nchini China, kongamano hilo lililoandaliwa kwa pamoja na Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang, na Kituo cha Utafiti wa Mikakati na Sera cha Sudan Kusini, liliwakutanisha kwa njia ya video maofisa wa serikali, wanadiplomasia, wataalamu na wajumbe wa mashirika ya kimataifa zaidi ya mia moja.

Kongamano la pili la Jumuiya ya Washauri Bingwa kati ya China na Sudan Kusini lafanyika kwa njia ya video_fororder_许镜湖

Akihutubia ufunguzi wa kongamano hilo, mjumbe maalumu wa serikali ya China anayeshughulikia mambo ya Afrika Balozi Xu Jinghu, alisema China inapenda kushirikiana na Sudan Kusini kuimarisha mawasiliano na ushirikiano kati yao kwenye nyanja za miundombinu, afya, elimu, upunguzaji wa umaskini, maendeleo endelevu na jumuiya za washauri bingwa, kuisaidia Sudan Kusini kuongeza uwezo wake wa kujiendeleza, na kusukuma mbele ushirikiano kati ya China na Sudan Kusini kwenye nyanja mbalimbali uendelee na kufikia ngazi mpya, ili kuwanufaisha kihalisi watu wa nchi hizo mbili.

Balozi Xu amepongeza kufanyika kwa kongamano hilo, na kuona kuwa “limefanyika kwa wakati na kuendana na hali halisi”. Anatumia kuwa kupitia kongamano hilo na majukwaa mengine, wasomi na washauri wa pande hizo mbili wanaweza kubeba wajibu wao unaotokana na mahitaji ya zama zilizopo, kukusanya mawazo bora, kufundishana na kushikilia lengo la msingi ambalo ni “kutoa busara, kutafuta maendeleo, kutatua matatizo na kuhimiza mshikamano”, ili kuweza kutoa mchango mkubwa zaidi kama washauri, na kutoa mapendekezo ya kisayansi na yanayotupia macho siku zijazo kuhusu nyanja za vipaumbele vya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, miradi muhimu na mbinu bora ya ushirikiano, na hivyo kuchangia busara zao kwa ajili ya maendeleo ya uchumi na jamii ya Sudan kusini, na vilevile maendeleo ya uhusiano kati ya China na Sudan Kusini.

Kongamano la pili la Jumuiya ya Washauri Bingwa kati ya China na Sudan Kusini lafanyika kwa njia ya video

Kongamano la awamu ya kwanza la Jumuiya ya Washauri Bingwa kati ya China na Sudan Kusini lilifanyika mwaka 2019 katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba, na sasa limekuwa jukwaa muhimu la mawasiliano na ushirikiano kati ya wasomi na wataalamu wa nchi hizo mbili.

Kituo cha Utafiti wa Afrika Kusini kilicho chini ya Taasisi ya Utafiti wa Afrika ya Chuo Kikuu cha Ualimu cha Zhejiang pia kilizinduliwa rasmi kwenye ufunguzi wa kongamano hilo.