Balozi Hua Ning: ushirikiano wa China na Sudan Kusini wapaswa kutoa kipaumbele katika kuboresha maisha ya watu
2021-12-20 09:53:11| CRI

Balozi Hua Ning: ushirikiano wa China na Sudan Kusini wapaswa kutoa kipaumbele katika kuboresha maisha ya watu

Balozi wa China nchini Sudan Kusini Bw. Hua Ning amesema ushirikiano kati ya China na Sudan Kusini unapaswa kutoa kipaumbele katika kuboresha maisha ya watu na kuhimiza maendeleo ya kilimo.

Akihutubia kwa njia ya video kwenye Kongamano la pili la Jumuiya ya Washauri Bingwa kati ya China na Sudan Kusini lililofanyika Disemba 17, Balozi Hua Ning ametoa mapendekezo sita kuhusu ushirikiano kati ya China na Sudan Kusini katika siku zijazo. Amesisitiza umuhimu wa kutoa kipaumbele katika kuboresha maisha ya watu na kuendeleza sekta ya kilimo. Amesema, suala kubwa linalohusiana na maisha ya watu nchini Sudan Kusini kwa sasa ni suala la usalama wa chakula. Sudan Kusini yenye eneo kubwa la ardhi ya rutuba linalofaa kwa kilimo, ina mustakbali mkubwa wa maendeleo ya kilimo. Katika miaka ya karibuni, China imejitahidi kutoa vifaa na mashine za kilimo pamoja na mafunzo ya teknolojia za kilimo kwa Sudan Kusini. Amesema, chini ya Mradi wa Kupunguza Umaskini na Kunufaisha Wakulima ambao ni moja kati ya Miradi Tisa ya ushirikiano iliyotangazwa na Rais Xi Jinping wa China kwenye mkutano wa nane wa mawaziri wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC, China itaendelea kuimarisha ushirikiano wa kilimo na upande wa Sudan Kusini, kuisaidia nchi hiyo kuongeza uzalishaji wa kilimo ili kutatua hatua kwa hatua changamoto ya kuwalisha wananchi, na kuyafanya mashamba yenye rutuba yawe “maghala ya chakula”.

Balozi Hua Ning: ushirikiano wa China na Sudan Kusini wapaswa kutoa kipaumbele katika kuboresha maisha ya watu

Mbali na kuendeleza kilimo, balozi Hua Ning pia amependekeza kuboresha mazingira ya kibiashara nchini Sudan Kusini, kupanua mawasiliano ya kibiashara kati ya pande hizo mbili, kuimaisha ujenzi wa uwezo haswa kwa vijana, kusukuma mbele mchakato wa amani na kuhimiza mawasiliano na ushirikiano kati ya wasomi na wataalamu wa China na Sudan Kusini, ili kuchangia busara zao kwenye ushirikiano wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.