Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema mshikamano na wahamiaji ni muhimu zaidi katika zama hizi
2021-12-20 09:03:36| CRI

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa asema mshikamano na wahamiaji ni muhimu zaidi katika zama hizi_fororder_timg (5)

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema, kuonyesha mshikamano na wahamiaji ni muhimu zaidi katika zama hizi.

Katika ujumbe wake wa maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi inayoadhimishwa Desemba 18 ya kila mwaka, Guterres amesema, wahamiaji wanaendelea kutengwa, kukosa usawa, na kukabiliwa na chuki na ubaguzi wa rangi, huku wanawake na wasichana wakiwa katika hatari kubwa ya kukumbwa na ukatili wa kijinsia.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, mwaka jana, karibu watu milioni 281 wamekuwa wakimbizi, ikiwa ni asilimia 3.6 ya idadi ya watu duniani.