Mkoa wa Xinjiang wapata maendeleo ya kasi
2021-12-21 09:22:32| cri

Mkoa wa Xinjiang wapata maendeleo ya kasi_fororder_赵立坚

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Zhao Lijian amesema, bila kujali kelele za wanasiasa wa Marekani, mkoa wa Xinjiang utapata maendeleo ya kasi zaidi.

Kauli hiyo imekuja baada ya Mabaraza ya bunge la Marekani hivi karibuni kupitisha Mswada wa Kuzuia Kulazimisha Wauyghur Kufanya Kazi.

Zhao amesema, wanasiasa hao wanapaswa kufuatilia zaidi mambo ya nchi yao, kwani hivi sasa nchini Marekani kuna wafanyakazi watoto takriban laki tano, huku wanawake na watoto kati ya laki 2.4 na 3.25 wakiteswa kama watumwa wa kingono. Zaidi ya hayo, katika miaka mitano iliyopita, idadi ya watu waliouzwa nchini Marekani kufanya kazi ya kulazimishwa kwa mwaka inafikia laki moja.