Mjumbe wa Umoja wa Mataifa yuko tayari kuitisha kikao kipya cha Kamati ya Katiba ya Syria
2021-12-21 08:52:52| CRI

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Syria Geir Pedersen amesema yuko tayari kuitisha kikao cha saba cha Kamati ya Katiba, iliyopewa jukumu la kuandaa katiba mpya kwa ajili ya nchi hiyo.

Akizungumza katika kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana jumatatu, Pedersen amesema yeye pamoja na timu yake wanashirikiana kikamilifu na serikali ya Syria na upande wa upinzani ili kuitisha tena kikao cha Kamati hiyo.

Amesema Syria imeendelea kukumbwa na ukosefu wa amani, na kuwa kituo cha wapiganaji wa kujitolea, wauzaji wa dawa za kulevya, na ugaidi.