Kiwango cha maendeleo ya vijana duniani chainuka kwa udhahiri
2021-12-21 13:18:04| Cri

Hivi karibuni China imetangaza Ripoti kuhusu maendeleo ya vijana duniani ya mwaka 2021, ikionesha hali ya sasa, mwelekeo na matatizo yaliyopo katika maendeleo ya vijana wa nchi mbalimbali duniani.

Ripoti hiyo imeonesha kuwa kiwango cha maendeleo ya vijana wa nchi mbalimbali kinaendana na kiwango cha maendeleo ya uchumi na jamii. Katika miaka ya hivi karibuni, kiwango cha maendeleo ya vijana katika nchi mbalimbali kimeinuka kwa udhahiri.

Ripoti hiyo pia imeonesha kuwa nchi zote zinaweka mkazo mkubwa katika utoaji wa ajira kwa vijana, na kupata maendeleo katika kuhimiza ushiriki wa vijana katika mambo ya umma.