Waziri wa mambo ya nje wa China aelezea uhusiano wa kidiplomasia na nje katika mwaka 2021
2021-12-21 11:00:40| cri

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi Jumatatu alitoa hotuba kwenye kongamano lililohusu hali ya kimataifa na uhusiano wa China na nchi za nje katika mwaka 2021, ambapo alisema katika mwaka uliopita dunia ilishuhudia janga linaloendelea na ambalo limeshindwa kudhibitiwa na kuongeza kasi ya mabadiliko ambayo hayajawahi kuonekana kwa karnea.

Bw. Wang amesema China siku zote inasimama upande sahihi wa historia, upande wa kuhimiza maendeleo ya binadamu, usawa na haki duniani na maslahi ya nchi mbalimbali zinazoendelea.

Alisema kwa diplomasia ya China katika mwaka uliopita, mwongozo imara zaidi wa utekelezaji ni diplomasia ya kiongozi wa nchi, na kauli mbiu ni kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja, huku mada kuu ikiwa ni kuiambia dunia hadithi za watu wa China na Chama cha Kikomunisti cha China, na kipengele dhahiri zaidi ni kukabiliana na mabadiliko kwa njia inayofaa na kupata maendeleo.

Bw. Wang alisema wakati janga la COVID-19 likiendelea, China imekuwa na diplomasia ya kupambana na janga hilo pamoja na nchi mbalimbali duniani kwa kutekeleza majukumu yake na imeshikilia uhusiano halisi wa pande nyingi kwa kutetea mamlaka ya Umoja wa Mataifa na utulivu wa utaratibu wa kimataifa.