Marekani inapaswa kukiri uhalifu wake wa kuua raia katika nchi za nje kwa vitendo halisi
2021-12-22 08:01:16| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana amesema, mauaji yaliyofanywa na jeshi la Marekani dhidi ya raia katika vita yake nje ya nchi yanapaswa kuchunguzwa kwa makini na kuadhabu wahalifu, ili kutubu uhalifu wake kwa vitendo halisi.

Bw. Zhao Lijian amesema, kwa muda mrefu sasa, Marekani inashikilia mtazamo wa umwamba, kupuuza demokrasia ya nchi nyingine kwa visingizio vya demokrasia na haki za binadamu, pia inakiuka haki za bindamu za nchi nyingine.

Vyombo vya habari vya Marekani vinasema, katika miaka mitano iliyopita, jeshi la Marekani limefanya mashambulizi zaidi elfu 50 ya anga katika nchi za Afghanistan, Iraq na Syria, na kusababisha vifo vya maelfu ya raia wa nchi hizo wakiwemo watoto.