Idadi ya vifo kutokana na mlipuko wa lori la mafuta nchini Haiti yafikia 90
2021-12-22 08:17:11| cri

Idadi ya watu waliofariki kufuatia mlipuko wa lori la mafuta katika mji wa Cap-Haiti kaskazini mwa Haiti imeongezeka na kufikia 90.

Habari zinasema, baada ya lori hilo kuanguka, baadhi ya watu walikimbilia kwenye eneo la ajali ili kuchota mafuta. Lori hilo lililipuka na kusababisha idadi kubwa ya vifo na majeruhi.