Rais wa China azungumza na Chansela wa Ujerumani kwa njia ya simu
2021-12-22 08:52:11| CRI

Rais Xi Jinping wa China amezungumza na Chansela wa Ujerumani Olaf Scholz kwa njia ya simu, akihimiza nchi hizo zijitahidi kukuza zaidi uhusiano wao.

Rais Xi amesema China inatilia maanani sana uhusiano wake na Ujerumani, na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ni mfano mzuri kwa ushirikiano kati ya China na nchi nyingine za Ulaya. Ametoa mapendekezo matatu kwa maendeleo ya uhusiano kati ya China na Ujerumani, ambayo ni kuwa na mwelekeo wa kimkakati katika kuendeleza uhusiano huo, kuhimiza ushirikiano wa kunufaishana kwa msimamo chanya na unaofuata hali halisi, na kushirikiana katika kukabiliana na changamoto, ili kutoa mchango mpya kwa usimamizi wa mambo ya kimataifa.

Scholz amesema anapenda kurithi urafiki na ushirikiano kati ya nchi yake na China, na Ujerumani inataka kujitahidi pamoja na China kuhimiza uhusiano wa wenzi wa kimkakati kwa pande zote kati yao kupata maendeleo zaidi.