WHO yasema mwaka 2022 utakuwa mwaka wa kumaliza maambukizi ya COVID-19
2021-12-22 08:15:16| CRI

WHO yasema mwaka 2022 utakuwa mwaka wa kumaliza maambukizi ya COVID-19_fororder_4

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetoa wito kwa dunia kuungana pamoja ili kumaliza janga la COVID-19 mwakani.

Shirika hilo limesema, tangu virusi vilivyobadilika vya Omicron vilipogunduliwa nchini Afrika Kusini, vimeenea katika nchi kadhaa, na kuongeza kuwa virusi hivyo ni hatari zaidi kuliko virusi vya Delta, vinaambukiza kwa kasi zaidi, na ni sugu dhidi ya chanjo.

Shirika hilo limesema, kutokana na sherehe za mwisho wa mwaka, ni muhimu sana kuchukua tahadhari na kujikinga.