Marekani inayowaua raia haina haki ya kuzungumzia haki za binadamu
2021-12-23 22:33:50| Cri

Hivi karibuni mwandishi wa habari Azmat Khan ametangaza ripoti yake ya uchunguzi kwenye Gazeti la New York Times la Marekani ikisema, katika miaka ya hivi karibuni, operesheni za kijeshi za Marekani katika Mashariki ya Kati zimesababisha idadi kubwa ya vifo vya raia wasio na hatia.

 

Hata hivyo, Ikulu ya Marekani haijajibu hadi sasa. Msemaji wa Kamandi Kuu ya Marekani Bill Urban alisema : "Hata kukiwa na teknolojia bora zaidi duniani, makosa bado yatatokea... Tunajaribu kujifunza kutokana na makosa haya."

 

Wanasiasa wa Washington wanajua vizuri jeshi la Marekani limefanya uhalifu gani. Ndiyo maana wakati Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ilipotangaza kuchunguza suala hili mwezi Septemba mwaka jana, rais wa wakati huo wa Marekani alikataa hadharani na kuwawekea vikwazo maafisa wawili waandamizi wa mahakama hayo.

 

Kama ripoti iliyotolewa na Taasisi ya utafiti kuhusu haki za binadamu ya China ilivyosema, “Historia imethibitisha kuwa, njia ya demokrasia ambayo Marekani inajaribu kutekeleza katika baadhi ya nchi, sio tu imeshindwa bali imeleta hasara za kibinadamu.”