China yapinga kithabiti mpango wa kumwaga baharini maji taka ya nyuklia kutoka kituo cha Fukushima
2021-12-23 08:57:29| CRI

China yapinga kithabiti mpango wa kumwaga baharini maji taka ya nyuklia kutoka kituo cha Fukushima_fororder_赵立坚

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Zhao Lijian jana amesema, China inafuatilia na kupinga kithabiti uamuzi wa Japan kumwaga maji taka ya nyuklia baharini.

Bw. Zhao amesema, tangu mwezi Aprili mwaka huu, jumuiya ya kimataifa imetoa malalamiko mengi kwa Japan kuhusu suala la kumwaga maji taka ya nyuklia baharini, lakini Japan imeendelea kudai kuwa, uamuzi huo ni salama.

Bw. Zhao ameongeza kuwa, kushughulikia maji taka ya nyuklia ya Fukushima kunahusiana na mazingira ya baiolojia ya bahari na afya ya umma duniani, na si jambo pekee la Japan. Amesema Japan inapaswa kusikiliza na kujibu ufuatiliaji wa jumuiya ya kimataifa zikiwemo nchi jirani zake, na kusitisha uamuzi huo. Ameongeza kuwa, Japan haiwezi kumwaga maji taka ya nyuklia baharini bila ya kufikia maafikiano na pande husika na mashirika ya kimataifa,.