Mkurugenzi wa WHO asema program za dozi ya tatu ya COVID-19 huenda zikaongeza muda wa janga hilo
2021-12-23 08:54:19| CRI

Mipango ya kutoa dozi ya tatu ya chanjo ya COVID-19 inaweza kuongeza uwepo wa janga hilo badala ya kulimaliza, ikiwa ni matokeo ya kukosekana usawa katika mgao wa chanjo kati ya nchi tajiri na masikini.

Hayo yamesema jana na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Dr. Tedros Ghebreyesus alipozungumza na wanahabari. Amesema kupeleka chanjo katika nchi ambazo tayari zina kiwango kikubwa cha asilimia ya watu waliopata chanjo kunatoa fursa kwa virusi hivyo kuendelea kuenea na kubadilika.

Amesema, awali, Shirika hilo lilitoa wito kwa nchi kufikia lengo la kutoa chanjo kwa asilimia 40 ya watu wake itakapofika mwisho wa mwaka, lakini ni nusu ya nchi wanachama wa WHO waliotimiza lengo hilo, na kuongeza kuwa, hali hiyo imesababishwa na ukosefu wa usawa katika ugawaji wa chanjo.