Wanawake wanavyosherehekea sikukuu ya Krismas
2021-12-24 09:04:44| CRI

Tarehe 25 Desemba ya kila mwaka, wakristo kote duniani wanaungana kusherehekea sikukuu ya Krismas, ambayo ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristu. Sote tunafahamu kuwa, kwenye sherehe zozote zile, mwanamke anachukua nafasi muhimu kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa. Watoto wamepata nguo mpya, chakula kipo, nyumba safi, na mambo mengine kama hayo.

Katika kipindi hiki cha Ukumbi wa Wanawake hii leo, tutazungumzia jinsi baadhi ya wanawake wanavyosherehekea sikukuu hii, kutoka Afrika hadi Marekani, na hata hapa China.