Taasisi ya haki za binadamu ya China yatoa ripoti kuhusu hatua za kisiasa za haki za binadamu za Marekani zinavyoharibu msingi wa utawala bora wa haki za binadamu
2021-12-27 16:24:38| CRI

Taasisi ya haki za binadamu ya China leo imetoa ripoti ya utafiti kuhusu hatua za kisiasa za haki za binadamu za Marekani zinavyoharibu msingi wa utawala bora wa haki za binadamu.

Ripoti hiyo imesema ili kulinda maslahi ya kisiasa na hadhi ya mwamba duniani, Marekani imefanya haki za binadamu kuwa suala la kisiasa katika sekta ya kimataifa ya haki za binadamu, hali ambayo imeharibu msingi muhimu wa kuhimili na kuendesha usimamizi wa haki za binadamu duniani, na kuleta tishio kubwa kwa maendeleo ya shughuli za haki za binadamu duniani na kusababisha matokeo mabaya.

 

Ripoti hiyo imesema Marekani inalichukulia suala la haki za binadamu kama nyenzo ya kisiasa, huku ikiamua msimamo wake kuhusu haki za binadamu kutokana na uhusiano kati ya haki hizo na mikakati yake ya kisiasa. Wakati ikikabiliana na migongano kati ya mkakati wake na vigezo vya kimataifa vya haki za binadamu, Marekani inachagua kuacha kanuni za haki za binadamu na kulinda mwamba wake, ama kwa kufuata baadhi ya kanuni za haki za binadamu zinazoendana na maslahi yake ya kisiasa. Pia inatumia moja kwa moja haki za binadamu kama kisingizio cha kutishia nchi zinazoweza kuharibu maslahi yake ya kisiasa na kuingilia mamlaka ya nchi nyingine.