Bomu lajeruhi Waganda watano mjini Kampala
2021-12-27 10:11:02| CRI

Polisi wa Kampala nchini Uganda wamesema wanachunguza ajali kuhusu kipande cha bomu kilicholipuka na kujeruhi watu watano.

Kwenye taarifa yake polisi imesema tukio hilo lilitokea Ijumaa usiku baada ya mtoto kuchezea na kukifungua kipande hicho cha bomu, ambapo lilitoa mlipuko na kujeruhi watu watano nyumbani. Hivi sasa majaruhi majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa huko Mulango kwa matibabu. Polisi imeongeza kuwa wanachunguza ili kujua asili ya bomu hilo na timu yao ya uchunguzi imegundua vipande vya vilipuzi ambavyo vimepelekwa kwa wataalamu kuvichunguza zaidi.

Polisi pia imeitaka jamii kuripoti kwa malaka husika vifaa vyovyote ambavyo wanavishuku ili vishughulikiwe kwa usalama.