Mkutano mkuu wa mwaka wa kazi za vijijini wa China wafanyika Beijing
2021-12-27 10:11:37| CRI

China imefanya mkutano mkuu wa vijijini wikiendi hii mjini Beijing.

Mkutano huo umechambua hali ya hivi sasa na kazi zinazohusu masuala ya kilimo, maeneo ya vijijini na wakulima, na kuweka mpango wa mwaka ujao.

Kabla ya mkutano huo wa siku mbili, Rais Xi Jinping wa China aliendesha mkutano wa Kamati ya Kudumu ya Ofisi ya Siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) kuhusu mambo ya kilimo na kutoa hotuba muhimu, akisisitiza kuimarisha maendeleo thabiti katika sekta ya kilimo na maendeleo ya vijijini, katika kukabiliana na changamoto mbalimbali.

Pia ametoa wito wa kufanya juhudi za kulinda usalama wa chakula na maeneo ya kilimo, kufanya marekebisho ya kimuundo, kupanua upandaji wa soya na mazao ya mafuta, na kuhakikisha utoaji wa nyama za nguruwe, mboga na mazao mengine ya kilimo.

Rais Xi amesisitiza msingi wa ustawi wa vijijini ni kuimarisha mafanikio yaliyopatikana katika kupunguza umaskini.