China yatoa wito wa kupanua makubaliano na kutatua kwa njia mwafaka tofauti kwenye mazungumzo ya nyuklia ya Iran
2021-12-28 09:49:49| CRI

China yatoa wito wa kupanua makubaliano na kutatua kwa njia mwafaka tofauti kwenye mazungumzo ya nyuklia ya Iran_fororder_Iran

Balozi wa China kwenye Umoja wa Mataifa na mashirika mengine ya kimataifa mjini Vienna Wang Qun ametoa wito wa kupanua makubaliano, kutatua tofauti kwa njia mwafaka na kutafuta maendeleo mapya kwenye duru ya nane ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran yaliyoanza upya mjini humo jana.

Balozi Wang amesema, katika suala la nyuklia la Iran na masuala yanayohusu kutoeneza nyuklia, sera yaubwana na vigezo viwili haipaswi kutumiwa kwa ajili ya kutetea maslahi binafsi ya upande mmoja.

Shirika la Nishati ya Atomiki la Kimataifa IAEA limeeleza wasiwasi wake juu ya makubaliano yaliyofikiwa na Australia, Uingereza na Marekani AUKUS ambapo Uingereza na Marekani zitaiunga mkono Australia kutengeneza nyambizi inayoendeshwa kwa nguvu ya nyuklia, ikiwa ni mara ya kwanza kwa nchi isiyo na silaha za nyuklia kumiliki nyambizi ya nyuklia.

Balozi Wang amesema vikwazo havipaswi kutumiwa kama tishio la kawaida na Iran haipaswi kuwekewa vikwazo vipya wakati wa mazungumzo hayo.