China yazitaka nchi zinazohusika kutekeleza ahadi za utoaji wa chanjo
2021-12-28 09:47:40| CRI

China yazitaka nchi zinazohusika kutekeleza ahadi za utoaji wa chanjo_fororder_销毁疫苗

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Zhao Lijian amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, anatumai nchi zinazohusika zitatekeleza kwa vitendo halisi ahadi zao, kutoa chanjo nyingi zaidi zenye usalama na ufanisi kwa nchi zinazoendelea zikiwa ni pamoja na nchi za Afrika.

Habari zinasema kuwa, hivi karibuni Nigeria ililazimika kuteketeza chanjo milioni 1.06 za AstraZeneca ambazo muda wa matumizi umeshapita. Vyombo vya habari vimedokeza kuwa, muda wa matumizi wa chanjo hizo zilizotolewa na nchi za magharibi ulibaki wiki nne hadi sita wakati zilipofikishwa nchini Nigeria.

Akizungumzia suala hili, Bw. Zhao Lijian amesema, chanjo ni silaha kali ya kupambana na virusi vya Corona, pia ni matumaini ya kuokoa maisha ya watu. Hivi sasa hali ya maambukizi ya virusi bado inaendelea, hivyo amezitaka nchi zinazohusika kutekeleza kwa hatua halisi ahadi zao za utoaji wa chanjo, ili kuchangia katika mapambano ya binadamu dhidi ya janga hilo na kupata ushindi mapema.