Uongozi wa CPC wasisitiza kuimarisha imani ya kihistoria, umoja na nia ya kupambana
2021-12-29 09:53:26| CRI

Mkutano wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China CPC umesisitiza kuimarisha imani ya kihistoria, umoja na nia ya kupambana ya wanachama wa CPC.

Mkutano huo wa siku mbili unaohusu ukosoaji na kujikosoa, umetilia mkazo kuendeleza moyo wa waanzilishi wa Chama na kushikilia uzoefu wake wa kihistoria kwenye kazi yake ya karne nzima iliyopita. Katibu mkuu wa kamati kuu ya CPC Xi Jinping aliongoza mkutano huo uliomalizika jana Jumanne na kutoa hotuba muhimu.

Mkutano huo ulipitia ripoti ya Ofisi ya Siasa ya mwaka 2021 kuhusu utekelezaji wa maamuzi ya pande nane ya kuboresha mwenendo, pamoja na ripoti nyingine ya kushughulikia utendaji wa kanuni kwa ajili ya kanuni na kupunguza mzigo katika ngazi ya chini kwa mwaka 2021. Ripoti imesema mwaka 2021 ni muhimu katika historia ya chama na serikali.