Waziri wa mambo ya nje wa Iran asema mazungumzo ya Vienna yako katika “mchakato mzuri”
2021-12-29 09:55:58| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa Iran asema mazungumzo ya Vienna yako katika “mchakato mzuri”_fororder_4

Waziri wa mambo ya nje wa Iran Hossein Amir Abdollahian amesema mazungumzo yanayofanyika mjini Vienna, Austria kuhusu kurejesha makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 yanaendelea katika “mchakato mzuri”.

Akizungumza pembezoni mwa hafla ya Jumanne, Hossein alisema nchi yake ina waraka wa maandishi unaoshikiliwa na timu ya majadiliano ya Iran. Amekumbusha kuwa pande nyingine zinazohusu makubaliano hayo pia zinatilia mkazo kwenye masuala yaliyopangwa kwenye waraka huo, lakini zina maoni tofauti juu yake.

Ameongeza kuwa kama pande nyingine zikiwemo Ufaransa, Uingereza, China, Russia na Ujerumani zinaendelea na mazungumzo hayo kwa nia ya dhati, kutakuwa na uwezekano wa kufikia makubaliano mazuri katika siku za hivi karibuni.