Tukiwa sasa tumeingia kwenye mwaka mpya wa 2022 kuna mambo mengi ya kutafakari kuhusu maendeleo ya wanawake. Hatua kubwa zimefikiwa ili kumuendeleza mwanamke katika miaka iliyopita, lakini licha ya mafanikio hayo bado kuna mapungufu mengi tu yanayoshuhudiwa ambayo yanamkabili mwanamke na yanahitaji kurekebishwa na kupewa kipaumbele kikubwa katika siku zijazo. Hivyo katika kipindi cha leo tutaangazia matarajio ya wanawake kwenye suala zima la ajira hasa ajira zisizo rasmi na nini cha kufanya katika mwaka huu mpya ili kuendeleza na kumuwezesha mwanamke.