Watu 38 wafariki kwenye ajali ya kuporomoka kwa mgodi wa dhahabu kusini mwa Sudan
2021-12-29 09:49:58| CRI

Watu 38 wafariki kwenye ajali ya kuporomoka kwa mgodi wa dhahabu kusini mwa Sudan_fororder_3

Kampuni moja ya serikali ya Sudan jana ilitoa taarifa ikisema mgodi wa dhahabu ulioko jimboni Kordofan Magharibi, kusini mwa nchi hiyo uliporomoka na kusababisha vifo vya watu wasiopungua 38.

Taarifa hiyo imesema meneja mkuu wa Kampuni ya Maliasili ya Sudan ameomboleza vifo vya watu hao 38 waliokufa kutokana na kuporomoka kwa mgodi wa Umm Draisaya, ambao uko karibu na mji wa El Nuhud jimboni Kordofan Magharibi, kilomita takriban 500 magharibi mwa mji mkuu Khartoum.

Kampuni hiyo imesema awali serikali ya jimbo la Kordofan Magharibi na Kamati ya Usalama ya jimbo hilo walitoa uamuzi wa kuufunga mgodi huo wakisema kwamba haufai kufanya kazi ya uchimbaji. Hata hivyo, wachimba madini wameendelea kuingia kisiri kwenye mgodi huo na kufanya kazi.