VOA na serikali ya Marekani washirikiana kuikandamiza China
2021-12-29 09:51:40| CRI

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Zhao Lijian amesema kwa muda mrefu sasa Sauti ya Amerika (VOA) imekuwa ikishirikiana na serikali ya Marekani kutangaza mambo mengi yanayohusu China kwa lengo la kuidhibiti na kuikandamiza China.

Akijibu ripoti ya mwisho wa mwaka iliyotolewa na VOA hivi majuzi ambayo inadai kwamba mwaka 2021 China ilidhoofisha haki za binadamu na utawala wa sheria wa Hong Kong na kutekeleza kile wanachokiita mauaji ya halaiki huko Xinjiang, Bw. Zhao amesema VOA siku zote inafumbia macho ukweli na kuifikiria vibaya China, hivyo ni vigumu kupata jambo zuri kuhusu China kwenye ripoti zao.

Msemaji Zhao ameeleza kuwa sio zamani sana, aliyekuwa mfanyakazi wa VOA alisema kuwa hakujua hadi alipokuja China kwamba ripoti za VOA alizokuwa akisoma kila siku zilikuwa kinyume kabisa na hali halisi ya China.

Kwa mujibu wa Zhao, mwandishi huyo pia amesema baadhi ya watu wanaofanya kazi VOA walifukuzwa kazi kwasababu wanashauri kuongeza habari zenye mtazamo chanya kuhusu China.