Nigeria yatangaza kutopokea chanjo za COVID-19 zitakazopitisha muda wa matumizi ndani ya muda mfupi
2021-12-30 09:46:22| CRI

Nigeria yatangaza kutopokea chanjo za COVID-19 zitakazopitisha muda wa matumizi ndani ya muda mfupi_fororder_尼日利亚头图

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Chakula na Dawa wa Nigeria Profesa Mojisola Adeyeye amesema, nchi hiyo haitapokea chanjo za COVID-19 zitakazopitisha muda wa matumizi ndani ya muda mfupi.

Siku hiyo Adeyeye ameeleza kuwa, Nigeria ilipata chanjo ya COVID-19 miezi kadhaa baada ya nchi zilizoendelea kuanza kutumia chanjo, kupitia mpango wa chanjo wa COVAX au msaada wa baadhi ya nchi, lakini baadhi ya chanjo hizo zilikuwa zinakaribia kupitisha muda wa matumizi ndani ya muda mfupi. Adeyeye ameeleza kuwa, Nigeria itashirikiana na wenzi wa kimataifa, kuhakikisha muda wa matumizi wa chanjo utafikia miezi mitano au sita.

Adeyeye pia ameongeza kuwa hivi sasa utafiti juu ya virusi vipya vya COVID-19 Omicron unaendelea duniani, na anawasihi wananchi wa Nigeria waendelee kufuata hatua za usalama zilizotolewa na idara za afya ili kuzuia kuenea kwa virusi hivyo.